Kampuni ya CPS imekuwa mshindi wa kwanza wa jumla katika kundi la walipakodi wa kati kwa upande wa kodi za ndani kutoka Unguja.
Mafanikio haya ni matokeo ya kuzingatia kanuni za ulipaji kodi ipasavyo huku dhamira ya kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. Tuzo hiyo ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa CPS, Bw Sebastian Dietzold akiandamana na Afisa Mkuu wa Uendeshaji CPS, Bibi Katrin Dietzold.
"Tulifikia hatua kubwa na hii na binafsi tunataka kutoa tuzo hii kwa timu yetu ya ajabu ya kifedha," Bi Dietzold alisema.
Aliongeza, "huu ni mwanzo tu. Muda si mrefu tutasimama pale pamoja na kampuni zetu zote. Kwa pamoja tunajenga taifa."
Wakati wa hafla hiyo tuzo ilitolewa kwa CPS na Mkurugenzi wa ICT na mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa IRA, Emmanuel Nnko.